Vichekesho vya Kesi ya Mmasai na MpareKulikuwa na wizi ulifanyika katika nyumba moja ya mpare pale hedaru na muhusika baada ya kufuatilia aligundua kuwa aliyemuibia ng’ombe wake alikuwa ni mmasai mmoja wa ng’ambo ya pili ya mto kikuletwa.
Mpare alimfungulia kesi ya wizi mmasai na mahojiano mahakamani yalikuwa kama ifuatavyo:
Mmasai; Wewe anasema mimi ameiba hiyo ng’ombe yako?
Mpare; Ndiyo
Mmasai; Aliingia kwa mlango ya nyuma ama ya mbele?
Mpare; Ya nyuma
Mmasai; Mekosa, aliingia kwa mlango ya mbele ya nyumba
Mmasai; Je, aliswaga ng’ombe dume akatangulia mbele au alikuwa nyuma?
Mpare; Dume alitangulia mbele
Mmasai; Mekosa tena, alibaki nyuma
Mmasai; Je ng’ombe alioibiwa iko ngapi?
Mpare; Ng’ombe  7
Mmasai; Amekosa kabisa, ng’ombe alikuwa 5 tu!!
Aha ha ha
Wewe hisi jaji alimhukumu au alimuachia huru huyo mmasai?

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.